ASIYESHINDWA BWANA YESU



kabla ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wangu nilikuwa naishi maisha ya machukizo mbele za Mungu nilikuwa mwongo,mwizi,mtu wa makwazo,mwenye hasira,wivu ,mzinifu na matendo mengine ya uchafu.



Nilipata neema ya wokovu mwaka 2008,kuanzia hapo Bwana alinitengeneza na kunifanya mtu wa pekee kabisa hapakuwa na yale mapando ambayo si ya kiMungu, maisha yalifanyika upya nikawa mtu wa kusoma neno na kulitafakari, nikawa mtii,mwombaji na mnyenyekevu kwa kila rika.



Hakika iko neema ya pekee ukiwa na Yesu Kristo ambae anaendesha maisha yetu kila wakati tukumbuke kuishi kwetu ni Ukristo shalom wana wa Mungu.

Like this story?
Join World Pulse now to read more inspiring stories and connect with women speaking out across the globe!
Leave a supportive comment to encourage this author
Tell your own story
Explore more stories on topics you care about